Msaada na Usaidizi
Pata msaada wa kutumia Huduma Mtandao: akaunti, malipo, Premium na huduma za serikali tunazounganisha.
Huduma Mtandao inafanyaje kazi
Huduma Mtandao inakusanya huduma za serikali na taasisi za Tanzania mahali pamoja. Kwa kila huduma tunaeleza inafanya nini na kukuunganisha na tovuti rasmi, ili usipoteze muda kutafuta.
Matatizo ya akaunti
Kama huwezi kuingia, tumia kiungo cha kubadilisha nywila kwenye ukurasa wa kuingia. Namba ya uthibitisho hutumwa kwenye barua pepe ya akaunti yako, hivyo angalia pia folda ya spam.
Malipo na Premium
Premium ni TZS 3,000 kwa mwezi na hulipwa kwa mitandao ya simu. Kama malipo yamekatwa lakini Premium haijaanza, wasiliana nasi na namba ya muamala tutashughulikia.
Kufuta akaunti
Unaweza kuomba kufutwa kabisa kwa akaunti na taarifa zako wakati wowote kupitia ukurasa wetu wa kufuta akaunti.
Wasiliana nasi
Tuma barua pepe [email protected] ukiweka barua pepe ya akaunti yako na maelezo mafupi ya tatizo.